Serikali imepiga marufuku rasmi utengenezaji na uuzwaji wa Pombe ambazo hufungwa katika vifungashio vya mifuko ya plastiki maarufu kama “VIROBA” na kuagiza kuanzia sasa watengenzaji wa pombe hizo watafute utaratibu uliotengenezwa na serikali kwa kuzifunga katika chupa zinazoweza kurejeshwa.
Agizo hilo linasema zinatakiwa kuwa na ujazo usiopungua milligram 250 ambapo atakayebainika kukiuka masharti ya kanuni hizi atawajibishwa kulipa faini, kufungwa jela au yote kwa pamoja kwa mujibu wa kanuni.
source: millardayo.com
0 comments:
Post a Comment