Sakata la dawa za kulevya bado lipo kwenye vichwa vya habari Tanzania ambapo Jumatatu ya February 20 2017 imemuhusu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe aliyefika Polisi kwa mahojiano.
Jioni ya Jumatatu Mbunge huyo wa Hai Kilimanjaro alichukuliwa na Polisi kwenye msafara wa magari yasiyopungua matatu ambapo iliripotiwa baadae kwamba Polisi walikwenda kufanya upekuzi kwenye nyumba zake Kawe na Mikocheni kwa mujibu wa Afisa habari wa CHADEMA.
Msemaji huyo wa CHADEMA Tumaini Makene alithibitisha Polisi kupekua nyumba zake na kuandikisha maelezo ya majirani ambapo akasema kwenye mida ya saa sita usiku huu Polisi wamemrudisha Mbowe kwenye kituo cha Polisi kati na wamemfungulia jalada la Uchunguzi…
source: http://millardayo.com/br20/
0 comments:
Post a Comment